The House of Favourite Newspapers

Uwoya: Pishi Langu Hachomoki Mtu

0


STAA wa filamu nchini Irene Uwoya, amesema kuwa kutokana na kujua kulihimili jiko vizuri, ni ngumu hata anapopata mpenzi kuchomoka kwa rahisi, kwa sababu habari yake anaijua na mwanaume siku zote ni kula chakula kizuri, mengine ni mbwembwe tu.

 

Akizungumza na Amani hivi karibuni staa huyo ambaye inadaiwa kuwa na mkwanja mrefu kwa sasa, alisema kuwa kitu kinachomlinda na kumuonesha yeye ni mwanamke sahihi, ni kwenye upande wa jiko.

 

Kwani halembi kabisa, anasimama kama mwanamke anayelijua jiko vilivyo.

 

“Huu mkono wangu ni hatari sana kwenye mapishi na ninakwambia, ukiingia huchomoki. Sasa sehemu yangu ninayojidai ndiyo hii, nikikupa pishi langu kubanduka kwenye himaya yangu, ni ngumu sana.

 

Lakini kitu kingine, sifa kubwa ya mwanamke ni jiko,” alisema Uwoya, huku akila nyama ambayo ameichoma nyumbani kwake.

Stori: Imelda Mtema

Leave A Reply