The House of Favourite Newspapers

UZEMBE! AWESO ‘AMPITIA’ MHANDISI WA MAJI MULEBA

Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Boniface Luhoko, baada ya kupokea mradi wa MAJI wa KATOKE bila ya kukamilika na ukidaiwa kujengwa chini ya kiwango na kampuni ya SAJAC LTD huku kero ya Maji ikiendelea kuwakabili wananchi wa Vijiji vya Kata ya Katoke wapatao 3,245 kwa kukosa Maji safi na salama.

Aweso amechukua maamuzi hayo baada ya Mradi huo wa Katoke Wilayani Muleba uliokuwa ukitekelezwa chini ya Mkandarasi M/S SAJAC INVESTEMENT Co. LTD wenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni 476, kushindwa kuwahudumia Wananchi hao, licha ya Serikali kumlipa mkandarasi huyo Shilingi Milioni 404 mpaka sasa.

Imeelezwa kuwa Sababu kubwa ya ukosefu wa Maji katika mradi huo ni kutokana na usimamizi mbovu uliopelekea Ununuzi wa vifaa visivyo na ubora na ujenzi wa miundo mbinu kwa kiwango cha chini, hali iliyopelekea mivujo ya mara kwa mara na kusababisha upotevu wa kiwango kikubwa cha Maji.

Tayari Mhandisi huyo amekamatwa na anashikiliwa na Jeshi la Polisi na Aweso kuagiza mkandarasi wa mradi huo atafutwe popote alipo baada ya kuandikiwa barua sita za wito na kushindwa kufika.

Aidha, NAweso ameagiza Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira (BUWASA) kutatua tatizo hilo haraka iwezekanavyo ili Wananchi hao wapate Maji safi na salama.

Aweso amehitimisha Wizara yake ya Kikazi ndani ya Mkoa wa Kagera Januari 13, 2019 kwa kupita wilaya zote za Mkoa huo.

Mradi huo ulioanzwa kujengwa mwaka 2013 ukitegemewa kukamilika mwaka 2014 kwa gharama ya shilling milion 476.

Comments are closed.