The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa BMM ngwasuma full vituko

0

Kama kawa kama dawa ni Ijumaa nyingine ambayo mapaparazi wetu wanaotii amri za mkuu wao, Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100,’ Dustan Shekidele ‘Mkude Simba, Mzee wa Mji Kasoro Bahari na Mpigapicha Mkuu, Richard Bukos ‘Mzee wa Chombo Kiendacho Kasi Mno’ walijiachia viwanja mbalimbali kusaka matukio na kuwasiliana Live Kidigitali na Mkuu wao aliyekuwa makao makuu ya gazeti hili yaliyopo Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam.

Saa 3:55 usiku

NJEMBA YANASWA IKIUZA SIMU FEKI UKUMBINI

Makao Makuu: Mkuu akiwa ofisini anaangalia saa yake na kubaini kuwa ni muda muafaka wa kuanza kuwasaka vijana wake waliotawanyika kona mbalimbali ambapo leo moja kwa moja anaanza na Dustan Shekidele ‘Mkude Simba, Mzee wa Mji Kasoro Bahari.’

Shekidele: Naam Mkuu wangu nakupata.

Makao Makuu: Vipi uko kiwanja gani na nini kinaendelea?

Shekidele: Salama Mkuu, niko maeneo ya Chamwino kwenye bar moja inaitwa Nyamatandala, Bendi ya Maisha Mapya inakamua.

Makao Makuu: Vipi kuna vituko gani ulivyovinasa?

Shekidele: Mkuu muda si mrefu kulikuwa na mzozo, kuna jamaa jana alimuuzia demu f,lani bonge la simu la Kichina sasa huyu demu alipoenda kumuonesha bwana’ake huyo bwana akamgutusha kuwa simu hiyo ndiyo miongoni mwa zile simu feki ambazo mwisho wake wa kutumika ni mwezi wa sita mwaka huu. Hivyo wakaanza kumsaka awarudishie pesa zao nakufanikiwa kumnasa hapa akila raha na mpenzi wake, ndiyo wamemkamata wanamdai awarudishie pesa zao achukue simu yake lakini jamaa naye mtata ile mbaya, hivyo kulikuwa na kajivarangati lakini waungwana wameingilia kati na kuwashauri wakamalizane polisi ili wawaache wengine waendelee kujilia raha zao.

Makao Makuu: Dah! Kipindi hiki unatakiwa umakini sana katika ununuzi wa simu. Oke Shekidele piga kazi.

Saa 5:46 usiku

UZINDUZI WA BMM NGWASUMA FULL VITUKO

Makao Makuu: Haya Bukos natumai unanipata.

Bukos: Nakupata Mkuu wangu.

Makao Makuu: Haya nieleze uko wapi na nini kinaendelea?

Bukos: Mkuu niko Mzalendo Pub hapa Jengo la Millennium Tower kwenye uzinduzi wa hii bendi mpya ya BMM Ngwasuma ambayo inaundwa na wanaumuziki wakongwe kama Mulemule, Totoo Zebingwa, Didier Namba, Mamaa Nzawisa na wengine kibao.

Makao Makuu: Vipi mambo yakoje hapo?

Bukos: Mkuu hapa vituko kibao, kuna mdada  alikuwa akijishaua na wigi lake kwenye kunengua bahati mbaya wigi likamuanguka dah! Kumbe ana bonge la upara na mapunye kibao kichwani, inaonekana kabisa ni mgonjwa, acha watu waanze kumcheka. Poa Bukos.

Saa 7:11 usiku

NJEMBA YACHEZEA KICHAPO UKUMBINI

Makao Makuu: Issa Mnally ‘Mzee wa GX 100’ haya pande za wapi?

Mnally: Mkuu niko Mbagala ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live.

Makao Makuu: Safi sana, vipi kuna nini hapo leo?

Mnally: Hapa Mkuu ni kujirusha tu raha zote za dunia ziko hapa.

Makao Makuu: Oke, nakutakia starehe njema ndani ya Dar Live. Ukitoka hapo wapigie wenzako uwaambie mkapumzike.

Mnally: Ha ha ha… Sawa Mkuu.

Leave A Reply