The House of Favourite Newspapers

Uzinduzi wa K-Vant wafanyika Mwanza

Mkuu wa wilaya ya Ilemela na watendaji wakuu wa Mega Beverages Company Limited  wakiwa na baadhi ya mawakala na wageni waalikwa.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt. Seveline Mathias (katikati) akiwa na Meneja Masoko na Mauzo wa Mege Beverages Company Limited, Marco Maduhu  (kushoto) na mmoja wa wakurugenzi, James Kimaro, wakati wa uzinduzi wa chupa mpya za K-Vant jijini Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela na watendaji wakuu wa Mega Beverages Company Limited  wakiwa na baadhi ya mawakala na wageni waalikwa.

 

KAMPUNI ya Mega Beverages Company Limited ya mkoani Arusha, inayotengeneza pombe kali chapa maarufu ya K- Vant,  imezindua chupa mpya za kinywaji cha K-Vant zenye mwonekano tofauti na chupa za awali katika jiji la  Mwanza, katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Golden Crest. Uzinduzi huo unafanyika baada ya uzinduzi rasmi mkubwa uliofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha.

 

 

 Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dk. Seveline Mathias, ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa serikali itaendelea kuuga mkono wawekezaji wa ndani ya nje ili kufaikisha mkakati wa kuifanya Tanzania nchi ya Viwanda.”Nawapongeza Mega Beverages Company Limited, kwa kuzindua chupa mpya sambamba na mkakati wenu wa kuyateka masoko zaidi,”alisisitiza.

 

 

 Meneja Masoko na Mauzo wa Mega Beverages Company Limited, Marco Maduhu, alisema mabadiliko hayo hayabadilishi ladha  halisi ya kinywaji hicho , wateja wake wataendelea kufurahia kutumia K-Vant, ikiwa katika ladha yake halisi ya siku zote.

 

 

 “Leo tunayo furaha kufanya uzinduzi wa chupa mpya ya K-Vant hapa mkoani Mwanza, Uzinduzi huu unahusisha mikoa yote ya kanda ya ziwa ambako kuna soko kubwa la bidhaa yetu ya K-Vant,tunawashukuru mawakala na wateja wetu wote ambao kwa muda  mrefu  wamekuwa wakituunga mkono na kutuwezesha kuendelea kupata mafanikio zaidi,”alisema Maduhu.

 

 

 Maduhu, aliongeza kuwa kampuni imejipanga  kuteka masoko zaidi ya ndani na kanda ya Afrika Mashariki,hali itakayosababisha kupanda kwa uzalishaji na  kuongeza pato la taifa kupitia kodi mbalimbali  sambamba na kunufaisha watanzania wengi kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

 

 

  “Mega Beverages Company Limited tutaendelea kuunga mkono jitihada za serikali  ya awamu ya tano za kufanikisha mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda sambamba na kuendelea kusaidia kukabiliana na changamoto za kijamii kwenye maeneo mbalimbali ya biashara zetu’’,alisisitiza.

 

 Alimalizia kwa kusema kuwa wakati uzinduzi wa chupa mpya unaendelea kufanyika,tayari kinywaji hicho kimeanza kusambazwa katika masoko .“ Wateja wetu wote popote mlipo tunawashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono nasi tutaendelea kuboresha huduma zetu za usambazaji na kuhakikisha kinywaji  bora cha K-Vant kinawafikia popote mlipo kikiwa katika chupa mpya”alisema Maduhu.

Comments are closed.