The House of Favourite Newspapers

Vanessa Mdee Mama Kijacho, Aanika Kibendi Chake

0

MIONGONI mwa headlines za mastaa zinazotikisa Bongo leo ni hii exclusive ya Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ambaye ameamua kuanika mimba yake.

Imekuwa ni stori za muda mrefu akitajwa kuwa Vanessa anayeishi Marekani na mpenzi wake, ni mjamzito lakini amekuwa akikanusha mara kwa mara taarifa hizo, leo amemaua kutuwekea picha za kutosha kupitia ukurasa wake wa Instagram na kututhibitishia kuwa muda wowote kuanzia sasa ataitwa MAMA, hii imeondoa maswali yote ambayo mashabiki wake wamekuwa wakijiuliza.

Vee Money ameonekana katika picha hizo akiwa na mchumba wake ambaye ni msanii maarufu wa Movie na Muziki nchini Marekani mwenye asili ya Nigeria, Rotimi huku wakifurahia matarajio mazuri ya kupata mtoto wao hivi karibuni.

Vanessa amemshukuru Mungu kwa ujauzito wake huku akiikabidhi familia yake ijayo kwa Mungu. Mastaa na watu mbalimbali wamempongeza Vanessa kwa hatua hiyo huku wakimuombea ajifungue salama.

 The greatest gift of all, THANKYOU JESUS for choosing us – it is a true true honor. We are overjoyed Isaiah 55:2 – All your children shall be taught by the LORD, and great shall be the peace of your children 🤍

ASANTE BABA MUNGU WETU 🙏🏽

Leave A Reply