The House of Favourite Newspapers

Video Chafu ya Mchungaji Yavuja

0

DUNIA inaelekea kubaya au kuisha kabisa! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na yanayoendelea baada ya kuvuja kwa video chafu inayodaiwa ni ya Mchungaji wa Kanisa la El Gibbhor Delivarence Ministy lililopo Tabata jijini Dar, anayejulikana kwa jina la Master King Prophet John.

 

Video hiyo imeibua gumzo kubwa kwenye makundi ya WhatsApp ya viongozi wa dini kuwa ni jambo la kushtua kwa mtumishi wa Mungu anayesimama madhabauni kuubiri neno la Mungu.

 

Chanzo makini kililieleza Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, video hiyo imekuwa ikisambaa kwa kasi ya ajabu ambapo watumishi wenzake wengi wanayo, jambo ambalo limewashangaza na kujiuliza imekuwaje mtu wa Mungu kufanya uchafu huo.

 

“Kuna mzigo wa mchungaji umevuja…yaani ni aibu tupu! Sijui kama umeshawafikia hapo mjengoni kwenu (Global)? Kama bado ngoja niwafanyie mpango, maana inashangaza kwamba imekuwaje mtumishi wa Mungu anafanya vile, jiulize sisi ambao siyo watumishi wa Mungu tutafanya mangapi!” Kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina gazetini.

VIDEO MEZANI KWA IJUMAA WIKIENDA

Baada ya kupata habari hizo kutoka kwa chanzo makini, kilitupenyezea pia video hiyo ambayo inaonesha mambo machafu ambayo hayaandikiki gazetini.

 

Video hiyo inamuonesha mchungaji huyo akiwasiliana na mrembo kwa njia ya ‘video call’ ambapo wako kama walivyokuja duniani wakiwa wanafanya uchafu huo.

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, haukuweza kung’amua kama video hiyo imerekodiwa upande gani; upande wa mrembo au mchungaji huyo, lakini alama ya kuashiria mmoja wao alirekodi, inaonekana katika video hiyo.

 

MCHUNGAJI ANASEMAJE?

Baada ya kuishuhudia video hiyo chafu, IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Nabii John na kumueleza juu ya video yake hiyo chafu kuvuja ambapo mazungumzo yalikuwa hivi;

Ijumaa Wikienda: Mchungaji kuna video yako chafu inaonesha ukiwasiliana na mrembo, imetua hapa mezani kwetu, unaizungumziaje?

Mchungaji: Hee! Una video yangu…na picha?

 

IJUMAA WIKIENDA: Ndiyo mchungaji tunayo hapa mezani kwetu.

MCHUNGAJI: Sasa suala hilo liko mahakamani na jambo likiwa mahakamani, si unajua siruhusiwi kulizungumzia mpaka pale mahakama itakapotoa uamuzi juu ya wahusika, ndipo nitakuomba unitafute. Nitakwambia kila kitu. Subiri tu ndugu, kuwa mvumilivu.

 

IJUMAA WIKIENDA: Kesi iko mahakama gani mtumishi?

MCHUNGAJI: Iko mahakamani, wewe jua hivyo.

IJUMAA WIKIENDA: Huko mahakamani umempeleka nani?

MCHUNGAJI: Aliyeisambaza, sitaki kuzungumza sana, subiri mahakama ikimaliza tu nitawaita waandishi wa habari wote na nitasema ukweli wote.

 

IJUMAA WIKIENDA: Sasa baba Mchungaji, huoni kama video hii inakuchafua na kushusha hadhi yako katika jamii ikiendelea kusambaa?

MCHUNGAJI: Ni kosa kusambaza video hizi, Polisi wanafuatilia kila anayeposti, nisingependa mpendwa wangu uingie matatani.

 

IJUMAA WIKIENDA: Sawa mtumishi, nashukuru kwa ushirikiano wako.

MCHUNGAJI: Karibu sana, kama kuna jambo lolote usisite kunitafuta na kuniuliza.

IJUMAA WIKIENDA: Sawa, asante mtumishi wa Mungu.

IJUMAA WIKIENDA lilipata pia mkanda mwingine mpya unaomuhusu mchungaji huyo, lakini hata hivyo, bado linajiridhisha nao kabla ya kuruka nao hewani.

 

WACHUNGAJI WACHUKIZWA

Baadhi ya wachungaji waliozungumza na gazeti hili, walionesha kuchukizwa na jambo hilo, kwani linalenga kuchafua nyumba za ibada kwamba zinaongozwa na watu wa aina gani?

 

“Nisingependa kuingia kwa undani, lakini watumishi wa Mungu tunapaswa kuwa wasafi wa roho na mwili.

“Jambo hili linatujengea picha mbaya mbele ya waumini, ni jambo la kukemea,” alisema Nabii James Nyakia wa Kanisa la Jerusalem lililopo Kitunda jijini Dar.

 

TUJIKUMBUSHE

Hii si mara ya kwanza kwa watumishi wa Mungu kuingia kwenye kashfa kama hii, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima aliwahi kuingia kwenye kashfa hiyo, lakini hata hivyo, aliikanusha video hiyo kwa kile alichosema ‘imechezewa’.

STORI: GLADNESS MALLYA, DAR

Leave A Reply