The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Lowassa Asikitishwa na Serikali Kufuta Kongamano la Vyama vya Siasa

0

DAR ES SALAAM: MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amesikitishwa na kile alichokisema uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuzuia Kongamano la Demokrasia na Siasa za Ushindani lililolenga kuchambua demokrasia nchini.

Lowassa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari ohisini kwake jijini Dar es Salaam.

“Lengo la kongamano lilikuwa ni kuwaleta Watanzania pamoja kuzungumzia demokrasia. Tupingane bila kupigane. Tofauti za vyama vyetu zisitufanye tupigane wala kutengana.

“Nataka nieleze masikitiko yangu kwa hatua iliyochukuliwa na serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuvunja kongamano hilo, tunalaani kitendo hicho cha kuminya demokrasia, nia yetu lilikuwa njema ya kuzungumzia demokrasia. Kila mtu ana mawazo yake.

“Picha iliyowekwa na waandaaji kuhusiana na kongamano hili inanionesha nikiwa na Kinana (Abdulrahman Kinana ni Katibu Mkuu wa CCM) tukitabasamu. Hii ni nchi moja, watu wale wale, tusitofautishwe na u-Chadema au u-CCM. Naomba tuijenge nchi yetu kwa njia ya demokrasia, na kwa maelewano.”

Aidha, Lowassa aliyewahi kuwa waziri mkuu kwenye serikali ya Jakaya Kikwete ameitaka serikali itoe tamko kuhusu matatizo yanayowakumba wananchi mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha pamoja na walioathiriwa na ukame.

Ameitaka pia serikali kuwa na utu, huku akitolea mfano wa kuwafuta kazi watumishi wa umma 9,932 waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi.

VIDEO: Lowassa Asikitishwa na Serikali Kufuta Kongamano la Siasa

Leave A Reply