The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Makonda Agoma Kuomba Radhi Clouds Media Kwasababu Hizi Hapa

0
Kutoka Kushoto ni Ruge Mutahaba, Makamu Mwenyekiti TEF, Deodatus Balile na RC Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesisitiza kwamba kamwe hataomba radhi kufuatia sakata la kudaiwa kuvamia Clouds Media, akidai kwamba hakuwa amefanya kosa lolote na kwamba yeye na Ruge ni marafiki wa siku nyingi.

 

Makonda aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari, wakati wakieleza hatua zilizofikiwa katika usuluhishi wa mgogoro kati yake na Clouds Media chini ya Ruge Mutahaba, kufuatiwa kufungiwa kwake na vyombo vya habari kutochapisha au kutangaza habari zinazomhusu.

 

Ruge ma Makonda, baada ya kuwa na bifu kwa muda mrefu, hivi karibuni walipatanishwa na mheshimiwa rais, John Pombe Magufuli alipokuwa kwenye mkutano mkoani tanga ambapo aliwaita wote wawili jukwaani na kuwataka wamalize tofauti yao.

Leave A Reply