The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Mcheki R.O.M.A Mkatoliki Alivyorudi Darasani na Kufundisha Somo la Hisabati

0

RAPA namba moja Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ jana alitembelea shule ya Msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Rangi Tatu na kufundisha somo la Hesabu ambalo alikua akilifundisha awali kabla hajawa msanii.

Pamoja na kufundisha Roma alitoa msaada wa vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo ikiwa ni moja wapo ya nyanja za kutatua kero katika shule zetu.

Roma anatarajiwa kufanya shoo kabambe Dar Live, Idd Mosi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kupanda stejini tangu apatwe mkasa wa kutekwa na kuteswa!

Shoo ya Dar Live imepewa jina la #Nishushe Dar Live, itakutanisha mastaa wengine wakali, DARASA, MR BLUE, STAMINA, SNURA na wenine kibao.

Leave A Reply