The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Meneja Aliyewataja Wasanii Ushirikina Akumbwa na Mazito, Ahaha Kumsaka Gwajima

0

Zimepita siku kadhaa tangu Meneja Maneno aliyekuwa meneja wa wasanii wakubwa maarufu Afrika kwa sasa wakiwemo Diamond Platnumz na Rich Mavoko kuwataja wasanii watatu akidai kuwa walikuwa wakiamaini katika nguvu za giza akiwemo.

Sasa mkali huyo ambaye naye ameamua kuanza kuimba, amesema amekuwa amekumbwa na mazito yakiwemo mauzauza nyakati za usiku na hata akiwa na fahamu.

Meneja Maneno amesema hayo wakati akifanya Exclusive Interview na Global TV Online huku akieleza kuwa kutokana na visa hivyo, kwa sasa yuko mbioni kumtafuta Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili kumpa msaada wa maombezi.

Maneno amezungumzia pia ujio wake kwenye muziki na kile anachokumbuka kwa wasanii aliowahi kufanya nao kazi.

MSIKILIZE HAPA AKIFUNGUKA

Leave A Reply