The House of Favourite Newspapers

Video queens wa bongo imekula kwao!

0

KIDOA-61Kidoa

MIAKA ya nyuma kidogo, wasanii wengi wa muziki hususan Bongo Fleva walikuwa wakiandaa video za nyimbo zao hapahapa Bongo lakini siku za hivi karibuni kumekuwa na dhana kwamba ‘kichupa’ kikitengenezwa nje ya nchi kinakuwa bomba zaidi.

Wengine wanaenda mbali zaidi kwa kuamini kutengeneza video nje ya nchi kunawapa ‘connections’ kubwa kwani madairekta wanajuana na vituo vikubwa vya TV Afrika na hiyo inakuwa rahisi kwao kutanuka katika soko la kimataifa.

amber luluAmber Lulu

Dhana hiyo imewafanya wasanii wengi hasa wale walio na majina kukimbilia nje hasa Sauz kwa madairekta kama vile Godfather, Justin Compos, Nick na wengineo kutengeneza video zao.

Ninapozungumzia mastaa wakubwa namaanisha wasanii kama vile Ommy Dimpoz, Ali Kiba, Nay wa Mitego, Diamond, Shetta, AY na wengineo ambao tumekuwa tukiwasikia kila wakati wakienda nje ya nchi kwa ajili ya kuandaa video mbalimbali.

Wakati hali ikiwa hivyo, tukumbuke kuna wadada kibao Bongo ambao wameingia kwenye fani ya kuuza nyago kwenye video ‘Video Queen’ wakiamini kwamba kwa kufanya kazi na wasanii wakubwa, huenda wakapata fursa ya kujipatia mkwanja ambao ungewawezesha kuyaendesha maisha yao.

LULU DIVA (11)Lulu Diva

Akinadada hao ni kama vile Gigy Money, Kidoa, Amber Lulu, Erycah, Lulu Diva na wengineo. Hawa walipoibukia kwenye fani ya kuuza sura kwenye video mbalimbali, waliamini watatusua lakini maamuzi ya sasa ya wasanii wengi kwenda kufanya video nje, kumewafanya wakose soko.

Hivi karibuni nilimsikia Mwanamuziki Nay wa Mitego akiwasifia sana mavideo queen wa Sauz akidai wanajua zaidi kucheza na kamera kuliko wa Bongo.

erycahErycah

Anaeleza kuwa, wengi wa wasanii wa Bongo wanaokwenda nje kwa mfano Sauz kuandaa video, huwa hawasafiri na mavideo queen wa Bongo, wanakuta kila kitu kimeandaliwa huko na wanachopewa wao ni gharama ya video nzima hadi inakamilika ikijumuisha na malipo ya wadada wa kuinogesha video.

Hiyo sasa imesababisha mavideo queen waliokuwa wakitegemea kufanya video na wasanii wakubwa Bongo kukosa dili na sasa wengi wao wanabaki kutumika kwenye video za wasanii wasio na majina na kujikuta wakipata mkwanja mdogo tofauti na matarajio yao.

Gigy-money-(5)Gigy

MATOKEO YAKE SASA

Kutokana na mazingira hayo, wadada wengi waliokuwa na ndoto za kuifanya kazi hiyo ‘kiprofesho’ wameanza kukata tamaa na kugeukia madili mengine huku wengine wakidaiwa kutumia miili yao kujipatia kipato.

Wengi ukiwauliza wanasema, bado wanaamini wanaweza kufanikiwa kupitia kazi hiyo kwani wanaokwenda nje kwa ajili ya video ni wachache kuliko wanaofanya hapa Bongo.

“Yaani wala siyo ishu, dili bado tunapiga kama kawaida na hilo la wasanii kufanya video nje sidhani kama litanifanya nife na njaa,” alisema Lulu Diva.

MSIKIE GIGY

“Wasanii wanaokwenda kufanya video nje wanataka tufe kwa njaa lakini nawashauri waache kwani Bongo kuna mademu wakali wenye figa kuliko hao wa Sauz ambao hawana muonekano wa kudatisha.

“Sikatai wao kubadili mazingira lakini wajue sisi mavideo queen wa Bongo tuna vitu adimu, chukua video ambayo imetengenezwa Sauz na ya hapa Bongo angalia mademu waliotumika na walinganishe na sisi, lazima utaona za Kibongo zinavutia.”

ERYCAH

“Mimi sina shida, najua kwa muonekano wangu kazi zitakuja zenyewe.”

Ushauri wangu siwakatazi wasanii kwenda kufanya video nje lakini wakati mwingine siyo lazima kulazimisha. Zipo ambazo tunaziona hazina ubora, zinashindwa hata na zile zilizoandaliwa Bongo na wakati huo zimetumika pesa nyingi ambapo inadaiwa kwa Justin Compus siyo chini ya Milioni 40.

Lakini pia kuna kila sababu ya wasanii hao kuthamini vya kwao, wapo madairekta wazuri tu Bongo na wapo mavideo queen bomba na lokesheni kali, kuna haja gani ya kukimbilia nje?

Tukikomaa hapahapa tunaweza kufanya vitu vizuri tena kwa gharama ndogo na kufika mbali.

 

Leave A Reply