The House of Favourite Newspapers

Video: Rais Magufuli ‘Apagawa’ na Mauno ya Polisi Geita


RAIS John Magufuli leo amepata burudani murua kutoka jeshi la polisi lililokuwa likiimba, kucheza na kukata mauno kwa umahiri wa hali ya juu ambapo ilimbidi atoe neno la shukurani kwa washiriki wa burudani hiyo.

 

Hilo limejiri leo wakati akizindua nyumba za makazi ya askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambapo kauli yake iliwaacha wasikilizaji wake hoi kwa kicheko.

 

Akionekana ‘kuchenguka’ na alichoona, Magufuli alisema:  ‘’Vijana wako wa polisi ambao nawashabikia sana inawezekana hawajui, wanapiga nyimbo nzuri sana, sauti zao nzuri, nimeshangaa hata viuno wanajua kukatika vizuri sana.  Nilifikiri mmekodisha bendi, nikawa namuuliza IGP na huyo ni askari mbona kiuno kinazunguuka vizuri sana?’’ 

Comments are closed.