The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ashiriki Ufunguzi wa Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani- Qatar – (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) unaofanyika Doha nchini Qatar tarehe 04 Oktoba, 2022.

Rais ameungana na viongozi wengine duniani kushiriki ufunguzi wa Mkutano wa World Innovation Summit for Health 2022 unaofanyika Multaqa Centre – Doha nchini Qatar.

 Rais  Samia akiwa pamoja na viongozi wengine katika ufunguzi wa Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) unaofanyika Doha nchini Qatar tarehe 04 Oktoba, 2022.
Rais Samia akiwa na Kiongozi wa Taifa la Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kiongozi huyo Doha.
Rais Samia akisalimiana na viongozi mbalimbali kabla ya kuanza mazungumzo na Kiongozi wa Taifa la Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Doha nchini Qatar tarehe 04 Oktoba, 2022. Aidha, Rais Samia pamoja na mwenyeji wake wamezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano na Biashara baina ya Tanzania na Qatar.
Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na Kiongozi wa Taifa la Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani.
Rais Samia akiwa kwenye mazungumzo na Muanzilishi na Mwenyekiti wa Wakfu wa Qatar (Qatar Foundation ) Sheikha Moza binti Nasser, Doha nchini Qatar tarehe 04 Oktoba, 2022.

Leave A Reply