The House of Favourite Newspapers

Video: Rais Samia Azindua Barabara Ya Morocco – Mwenge

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefungua barabara ya Morocco – Mwenge yenye urefu wa kilomita 4.3 leo tarehe 05 Desemba, 2021.

 

Rais Samia amesema ujenzi wa barabara ya Morocco – Mwenge ulianza chini ya Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli na angetamani leo aone matunda ya jitihada zake lakini hayupo hivyo watanzania wamuombee pumziko la amani.

 

“Niombe sana, ndugu zangu wa Dar es Salaam kwa sababu nazungumza hapa Tanzania nzima, twende tukatunze miundombinu tunayoijenga, miundombinu hii huwa inajengwa kwa umri kadhaa, pesa inayotumika na kuweka barabara tunakisia utakwenda kwa umri kadhaa”

 

“Hivi karibuni tunafikiria ndani ya Serikali, kwenda kuiendeleza Jangwani, kwa njia tutakayokubaliana, kwa hiyo Dar es Salaam inabadilika, jinsi jiji linavyobadilika ndugu zangu, niwaombe sana na wananchi tubadilike, tubadilike kifikra, tubadilike kimatendo”.

 

“Watu wanatupa tu taka, hawajali kama mitaro ile itaziba au itapeleka maji, kuna watu mvua zikinyesha wamefungulia vyoo vyao na kumimina kwenye mitaro, bila kujali watoto wetu wakati mwingine watundu hawasikii, wanaingia kwenye mitaro ile wanakwenda kubeba maradhi”

 

“Nishukuru sana utamaduni wa Japan, wenzetu Japan ni utamaduni wao siku zote wakisalimiana wao hawapeani mikono, wanafunga mikono na kuinama, wameshasalimiana, na ndio utamaduni walioturithisha katika janga hili la Covid, ndugu zangu sio lazima tupeane mikono”  amesema Rais Samia leo Desemba 5, 2021 akifungua barabara ya Morocco – Mwenge Dar es Salaam.

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply