The House of Favourite Newspapers

Video: Waziri Wa Maji Awesu Amthibitishia Makonda Ndani Ya Wiki 3 Maji Kupatikana Katoro – Geita

0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda akiongea na Waziri wa Maji nchini Juma Aweso mbele ya wananchi.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda amempigia simu Waziri wa Maji, Juma Awesu na kumtaka kutolea ufafanuzi kero ya upatikanaji wa Maji safi na Salama katika Mji wa Katoro ulipo Kata ya Ludete Wilayani Geita mara baada ya kupokea changamoto hiyo kutoka kwa Wanachi hao aliozungunza nao njian akiwasili katika Mkoa wa Geita katika ziara yake ya Kikazi leo tarehe 11 Novemba, 2023.

Katika Majibu yake, Waziri Awesu amesema kuwa zilishatolewa fedha Tsh Bilioni 6.5 kwa mradi wa maji eneo hilo na mradi umeshavuka asilimi 90% na ndani ya wiki tatu mradi huo utakuwa umekamilika na Wakazi hao kunufaika kwa kupata maji safi na salama.

Aidha, Awesu amesema Geita Mjini kuna fedha zaidi ya Tsh Bilioni 128 na Chato zaidi ya Tsh Bilioni 38 kwa miradi ya maji katika miji ambapo amesema katika jumla ya Vijiji 436 tayari Vijiji 333 huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama imefika.

Naye Mwenezi Makonda amempongeza Waziri Awesu kwa maelezo yake na kumtaka kuhakikisha anatekeleza ili kukamilisha ahadi yake aliyoitoa kwa Wananchi hao kwani kuwadanganya ni sawa na kuifanya CCM ionekane inajinadi katika uongo.

Novemba 11, 2023 wakati aliposimama na kuzungumza na Wananchi wa Katoro katika Kata ya Ludete akiwa ziarani Mkoani Geita.

Leave A Reply