The House of Favourite Newspapers

Wakili Kambole: Watuhumiwa Mauaji Hupewa Mawakili Bure – Video

0

WATU  wenye makosa ya mauaji ndiyo pekee wanaopewa bure mawakili  na serikali, pia rais anapokuwa madarakani hawezi kushtakiwa na hata kipindi cha uchaguzi rais bado anakuwa madarakani sababu urais unakoma pale anapopatikana rais mwingine.

Hayo ni miongoni mwa mambo aliyoyasma wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole,  katika mahojiano wakatiwa   Kipindi cha Front Page kupitia +255 Global Radio, leo Mei 29, 2020, kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo kesi inayomkabili mchekeshaji Idriss Sultan.

Katika mahojiano hayo wakili huyo amegusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na mfumo wa uchaguzi nchini chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haki za binadamu, mfumo na uamuzi wa mahakama.

Alizungumzia pia makosa ya jinai ambapo alisema makosa hayo hufanywa zaidi na watu wa hali ya chini.

“Makosa mengi ya jinai yanafanywa na watu wa hali ya chini, huwezi ukakuta matajiri wanafanya makosa haya,” alisema na kuongeza pia kwamba sheria pia lazima ziende na wakati na eneo husika, jambo ambalo wanasheria wanakuwa katika nafasi bora zaidi kupigania mabadiliko yake.

Akizungumzia mfumo wa uchaguzi alisema, kwa mfano, sheria inayopinga kutokuwepo fursa ya kupeleka malalamiko mahakamani dhidi ya matokeo ya urais, ni sheria ambayo haina mlengo mwema katika uchaguzi huru.

Alisema pia mlundikano wa watu magerezani unasababishwa na kuongezeka kwa kesi ambazo hazina dhamana, na akasisitiza pia kwamba mtu akifungwa si kwamba ameonewa, au akishinda ndiyo kwamba hakutenda kosa aliloshitakiwa bali inawezekana kwamba ushahidi uliotolewa haukuwa na nguvu kumtia hatiani.

Kwa habari zaidi, sikiliza video hapa chini.

 

Leave A Reply