The House of Favourite Newspapers

Vijana 300 Wajitokeza Shindano La ‘Public Speaking’

0
Majaji wa Shindano la kusaka vipaji vya kuzungumza mbele ya hadhara ‘Public Speaking’, wakimkabidhi cheti cha kufuzu hatua ya pili mmoja wa washiriki wa shindano hilo.

ZAIDI ya vijana 300 wamejitokeza kushiriki Shindano la kusaka vipaji vya kuzungumza mbele ya hadhara ‘Public Speaking’  linalolenga kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuzungumza mbele za watu bila kuogopa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa waratibu wa shindano hilo ambalo limeratibiwa na kampuni ya Global Publisher’s, Pacific Ibrahimu alisema zaidi ya fomu 600 zilitolewa kwa washiriki mbalimbali nchi nzima.

Mratibu wa Shindano la kusaka vipaji vya kuzungumza mbele ya hadhara ‘Public Speaking’, Pacific Ibrahimu akizungumza na washiriki hao (hawapo pichani)

Alisema usaili wa awali ulioanza Februari 10 mwaka huu, ulishuhudia washiriki zaidi ya 300 ambao walionesha shauku na nia ya kutaka kujifunza na kunoa vipaji vyao.

 

“Dhumuni kubwa la kuanzisha shindano hili ni kuinua na kuendeleza vipaji vya watu ambao wana uwezo wa kufikisha ujumbe wao mbele za watu kwa njia mbalimbali.

“Tumeona watu wengi maarufu kama vile Erick Shigongo na Chris Mauki ambao wamekuwa wakihamasisha vijana kujitokeza kuonesha uwezo wao wa kuzungumza mbele zatu ili kutumia kipaji hicho kama moja ya njia ya kujiendeleza lakini bado hamasa hii haijatiliwa mkazo ndio maana tumeanzisha shindano hili,” alisema.

 

Alisema katika mzunguko wa pili washiriki hao watabaki 30 baada ya kuchujwa kulingana na vigezo ambavyo majaji watakuwa wamezingatia.

Leave A Reply