The House of Favourite Newspapers

Prof. Lipumba Ampa Tano Rais Magufuli, Amvaa Maalim Seif – (Video)

 

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema anaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli katika mpango wa ukusanyaji kodi, huku akitaka utekelezaji huo uzingatie uhalisia

 

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo wakati alivyokuwa anazungumza na waandishi wa habari baada ya ukimya wake wa muda mrefu na kusema Baraza kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitaka mamlaka inayohusika na masuala ya ukusaji wa kodi kwa wafanyabiashara wawe wanatoa makadirio mazuri ili kuweza kuwapa fursa wateja zao kulipa kodi vizuri.

 

“Baadhi ya makampuni na wafanyabiashara wanakadiriwa kodi kubwa kuliko wanachouza na hatimaye biashara zao zinafungwa. Baraza kuu la Chama cha Wananchi CUF linaitika serikali ifanye makadirio ya kodi ambayo yatakuwa yanazingatia hali halisi, Mamlaka ya kodi isiwakamua wafanyabiashara mpaka biashara kufungwa na kusababisha kupata hasara”, amesema Prof. Lipumba.

 

Pamoja na hayo, Prof. Ibrahim Lipumba ameendelea kwa kusema “tunaunga mkono katika ukosaji wa kodi lakini utekelezaji wake uzingatie hali halisi, tusije tukawakamua watu wanaofanya biashara, wenye makampuni ambao wanatoa ajira mpaka biashara na shughuli zao kupelekea kuzifunga”.

 

Kwa upande mwingine, Prof. Lipumba amedai Baraza kuu limepata kuwepo kwa malalamiko ya hali ya maisha kuwa magumu kupitiliza na kuiomba serikali iongeze mzunguko wa pesa ili kuweza kuinua maisha ya watanzania wa hali ya chini.

VIDEO: MSIKIE LIPUMBA AKIFUNGUKA

Comments are closed.