The House of Favourite Newspapers

VIDEO: AS Vita wavaa maski,wagoma kuingia vyumbani

 

AS Vita ya Congo jana ililazimika kuvaa maski za kuziba pua na kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla ya mechi kwa madai wameweka sumu.

 

Wachezaji hao pamoja na viongozi wao walikuwa wakilalama kwamba hewa sio nzuri na wanahujumiwa. Timu hiyo ikiongozwa na kocha mkuu wake, Florent Ibenge walikazimika kukaa kwenye korido na kufanya shughuli zao eneo hilo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra Dokta wa timu hiyo, Nowa Lelo, alisema kuwa walikuta hali isiyo ya kawaida mara baada ya kuingia vyumbani huku akidai kuwa waligundua kuwa chumba hicho kilipuliziwa sumu yenye athari kwa binadamu.

 

Lelo alienda mbali kwa kusema, dawa hiyo iliyopulizwa kwenye chumba hicho, hutumika kumpulizia maiti ili isiharibike, ingawa watu wa Simba walikuwa wakiwapuuzia.

 

“Tuna uhakika na hiki tunachokisema na kama kungekuwa na kipimo cha kuweza kupima ningepima ile hewa mbele yako na kukupa majibu, ila hakuna tatizo huu ndiyo mpira wetu wa kiafrika na tulijua kuwa haya yanaweza kutokea, ndiyo maana tukabeba hizi maski.

 

“Sisi ni wazoefu na soka la kiafrika tunajua hujuma zote, tutaenda kupambana na hakuna shida yoyote,” alisisitiza Lelo kabla ya mchezo huo.

STORI: ISSA LIPONDA

Comments are closed.