The House of Favourite Newspapers

VPL: Azam FC yaichapa Mtibwa

0

VPL-logo

Kikosi cha Azam FC leo kimeibuka kifua mbele baada ya kuichapa Mtibwa Sugar bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro.

Bao la Azam FC limefungwa dakika ya 62 na John Bocco kwa penalti, iliyotokana na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent kuunawa mpira ndani ya eneo la 18 kufuatia krosi ya Kipre Tchetche.

Kwa matokeo ya leo, Azama wamefikisha jumla ya pointi 55 wakiwa bado nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Yanga.

Leave A Reply