MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba, ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua.
Machungwa ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C. Pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya brokoli na pilipili kali.
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.
ASALI
Kama inavyojulikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua.
Asali inasaidia kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika unaweza kuitumia kama kinga kwa kulamba kila siku kijiko kimoja kikubwa inasaidia kukuimarisha kiafya.
MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha protini iliyonacho, mtindi unafaa sana kwa mtu anayesumbuliwa na mafua pamoja na kikohozi.
SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz