The House of Favourite Newspapers

Wabongo Wampa za Chembe Zari

0

 

DAR: ZILIPENDWA wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amejikuta ‘akipopolewa’ maneno makali na Wabongo kufuatia tabia yake ya kuwasema vibaya mitandaoni.

 

Ishu hiyo imekuja mara baada ya hivi karibuni mrembo huyo kuambiwa na mmoja wa mashabiki wa Kibongo kwamba, awaache kidogo kwani wapo kwenye majonzi ya msiba wa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini William Mkapa.

 

Alipoambiwa hivyo, Zari alimjibu vibaya shabiki huyo ndipo Wabongo walipomfungia kazi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

“Kwenda huko mwana kulitafuta mwana kulipata, we’ kila siku kuwasema Wabongo, wewe vipi wewe,” aliandika mdau mmoja huku wengine wakiunga kwa kumpa matusi mazito yasiyoweza kuandikika gazetini.

 

Wabongo hao walisema, bibie huyo amekuwa na kawaida ya kuwajibu vibaya Wabongo, hivyo wamemtolea uvivu ili akome kuwajibu vibaya.

 

Wengine walienda mbele kwa kukumbushia tukio lake la hivi karibuni ambapo aliwachana Wabongo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba, watoto wake wana akili tofauti na watoto wa Wabongo.

 

“Huyu ni mpuuzi tu, juzijuzi hapa alituletea zile za sijui wanae wana akili, kwani sisi wa kwetu hawana? Mjinga sana huyu,” alichangia mdau mwingine mtandaoni.

STORI: KHADIJA BAKARI, RISASI

 

Leave A Reply