The House of Favourite Newspapers

Wabunge Chadema Wagoma Kurudisha Posho kwa Ndugai

0

 WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameagizwa kutotii agizo la Job Ndugai, Spika wa Bunge kwamba warejeshe fedha za posho walizopewa. 

 

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema amesema, Kati Kuu ya chama hicho imetafakari na kuona kuwa, hakuna sababu ya wabunge hao kurejesha fedha hizo kama ilivyoamriwa na mahakama.

 

Tarehe 6 Mei 2020, Spika Ndugai aliwataka wabunge wa Chadema waliogoma kuhudhuria vikao vya bunge kwa kujiweka karantini, warejeshe fedha za posho walikopewa za Bunge.

Akisistiza agizo hilo Spika Ndugali alisema, endapo mbunge atakaidi agizo hilo, itamlazimu atakaporejea awe na cheti kinachoonesha amepima ugonjwa wa corona na majibu yake ama hatua zaidi zitachukuliwa.

 

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 11 Mei 2020, wakati akieleza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho, Mnyika amesema “Kamati Kuu imeagiza wabunge kutotekeleza maagizo hayo, kwa kuwa ni kinyume cha sheria.”

 

Amesema, Kamati Kuu kuu imejiridhisha kuwa wabunge wake wake si wezi na kwamba, fedha hizo hawajaiba hivyo hawana sababu ya kuzirejesha.

 

“Azimio la sita ni juu ya madai yaliyotolewa na Spika Ndugai, kwamba wabunge wa Chadema waliopewa posho za kujikimu za kuishi Dodoma ni wezi.

 

“Kamati imefikia uamuzi, kwamba madai haya ya spika ni ya uongo na kutoa rai kwa wabunge kutokutekeleza yale ambayo spika ameleekeza kinyume na Katiba na sheria za nchi,” amesema Mnyika.

 

Leave A Reply