Wabunge Waliofukuzwa Uanachama Chadema, Watingia Bungeni Leo – Video


Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameingia bungeni leo Ijumaa Mei 13, 2022 kuendelea na shughuli za Bunge jijini Dodoma.

 

Jumatano ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.

 

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment