The House of Favourite Newspapers

Wachezaji Simba Waandaa Sapraizi leo

Kikosi cha timu ya Simba.

WACHEZAJI wa Simba, wamesisitiza kwamba wataifanyia sapraizi ya aina yake AS Vita kwa kuipiga kwenye uwanja wake na hawataamini kitakachotokea.

 

Kiungo James Kotei raia wa Ghana, mwenye uwezo wa kucheza beki na kiungo mkabaji, anafahamu vizuri sana kwamba AS Vita Club ya DR Congo ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kufungwa na Raja Casablanca, lakini hilo

 

haliwatishi. “Tunaichukulia hiyo mechi kwa uzito mkubwa sana, tunataka pointi katika mchezo huo kwani ndizo zitatuweka sehemu nzuri zaidi. Wajiandae,” alisema Kotei.

John Bocco amewatoa hofu mashabiki; “Kwanza niwatoe hofu mashabiki wetu kwa sababu kazi ndiyo kwanza imeanza hatupaswi kuridhika na matokeo ya mchezo uliopita.

 

“Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa sababu ni timu kubwa na ina uzoefu wa kutosha lakini kwetu hakipaswi kuwa kigezo cha kuanza kuwahofia zaidi tunakwenda kwao kutafuta matokeo ili tuendelee kuwa katika nafasi nzuri kwenye michuano hii,” alisema Bocco.

SAID ALLY NA KHADIJA MNGWAI DAR ES SALAAM

Comments are closed.