Wadau Walivyoipongeza NIC Goba Hills Marathon
Wadau mbalimbali walioshiriki mbio za NIC Goba Hills Marathon wamezipongeza mbio zilizokuwa na lengo la kuimarisha afya zao pamoja na kusaidia kuchangia afya ya mama wajamzito na watoto.
Mbio hizo ziliwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali zifanyika Jumamosi iliyopita ambapo miongoni mwa walioshiriki ni Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Camilius Wambura aliyeshiki mbio za kilomita 10, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Building Works LTD, Mohamed Noray aliyeshiki mbio za kilomita 5 na wengineo.
Mbio hizo zilianzia Shule ya Sekondari ya Goba zikiwa na wakimbiaji wa viwango tofauti ambapo mbio ndefu zaidi ilikuwa ni kilomita 42 ambapo pia kulikuwa na mbio za kilomita 21 kilomita 10 na kilomita 5.
Baada ya kumaliza mbio hizo Noray aliwashukuru waandaaji wa mbio hizo pamoja na wadhamini wakuu Shirika la Bima la Taifa (NIC) ambazo zimewasaidia kuimarisha afya zao pamoja na kuchangia fedha kwaajili ya afya ya mama wajawazito na watoto.
SACP Camilius Wambura naye aliwasifu waandaji na waliojitokeza kwenye mbio hizo kwa umoja na amani waliouonesha na kujenga afya zao.
“Michezo kama hii ni muhimu sana katika jamii haswa kipindi hiki cha janga la Covid-19 kwani kwa zoezi kama hili ni zaidi ya kujifusha”. Alimaliza kusema SACP Wambura. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL