The House of Favourite Newspapers

Wafanyakazi Tanesco Wasimamisha Msafara Wa Shigongo Buchosa

0

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Buchosa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo akiwa njiani akitokea katika Kijiji cha Busenge jimboni humo, kuwafariji baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa baada ya mvua kubwa kunyesha iliyoambatana na upepo mkali uliopelekea kuezuliwa nyumba takribani 29 kuathirika na mvua hizo, amezuiliwa na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Buchosa.

Wakati mgombea huyo akielekea kwenye mkutano wa kampeni alikutana na wafanyakazi wa TENESCO wakielekea kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuchimbia nguzo za umeme ambao walisimamisha msafara wakimtaka Shigongo kuzungumza nao.

Shigongo ambaye siku zote amekuwa msikivu na mnyenyekevu kwa wote, alitii ombi la wafanyakazi hao kisha kusimama na kuzungumza nao.

“Nawashukuru sana kwa kuniamini na nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya katika kuijenga nchi yetu. Mimi nataka niwaeleze kwamba nchi yetu hii tutaijenga sisi wenyewe Watanzania hasa kwa kufanya kazi kama mnavyofanya.

“Usimdharau mtu yeyote kwa kazi anayoifanya, hivyo hiki mnachokifanya kitabaki katika historia ya vizazi vijavyo, nawaomba muendelee na moyo huo wa kuijenga nchi yetu Mungu awabariki sana,” alisema Eric Shigongo.

Leave A Reply