The House of Favourite Newspapers

Zuchu Awafunika Mastaa Bongo Ndani ya Miezi Mitano

0
Staa mpya wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ akiwa katika pozi na mabodigadi wake.

UNAAMBIWA hata inzi hakatizi mbele yake, kwani huo ulinzi aliowekewa staa mpya wa Bongo Fleva, Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’, siyo wa nchi hii, kiasi cha kuwafunika mastaa wote wa kike unaowajua Bongo hii.

 

MSITU WA MABODIGADI

Ili kumfikia Zuchu kwa sasa, inabidi ufanye kazi ya ziada kupenya kwenye msitu wa mabodigadi wakali kama pilipili kichaa wasiopungua sita, ambao wamekuwa wakiambatana naye kila anakokuwa.

Kali zaidi ambayo haijawahi kutokea Bongo, ni pale Zuchu anapokuwa kwenye mizunguko yake binafsi, kwani ulinzi si wa kitoto hata kama ameingia mgahawani, saluni au hata maliwatoni, lazima nje kuna njemba zilizojazia vifua, zikimlinda.

 

KUPIGA NAYE PICHA NI ISHU

Tofauti na ilivyozoeleka zamani, lakini sasa hata kupiga picha na Zuchu, imekuwa ni ishu au siyo kazi rahisi, kwani ni vigumu kumsogelea bila kukutana na kizuizi cha mabodigadi wake.

Faustina Charles ‘Nandy’.

 

AZIMA MBWEMBWE ZA AKINA WEMA

Uchunguzi unaonesha kwamba, zile mbwembwe zilizozoeleka za mastaa zilipendwa wa kike Bongo, hasa kutoka kwenye tasnia ya Bongo Movies kama Wema Isaac Sepetu, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na wengine, zimezimwa rasmi na msanii huyo, ambaye ni memba mpya wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).

Wema Isaac Sepetu

Ukiacha hao wa Bongo Movies, pia amefanikiwa kuwa tishio kwa mastaa wenzake wa kike wa Bongo Fleva, kama Faustina Charles ‘Nandy’, Esterlina Sanga ‘Linah’, Hamisa Mobeto, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Vannesa Mdee ‘V-Money’, Mariane Mdee ‘Mimi Mars’ na wengine kibao.

 

ANASTAHILI KUISHI KISTAA

Kwa mujibu wa wadau wa Bongo Fleva waliozungumza na mwandishi wetu katika mjadala mkali kuhusu mafanikio ya ghafla ya Zuchu, ambaye yupo chini ya WCB ya kinara wa muziki huo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, msanii huyo anajiwekea rekodi za kila aina, ndani na nje ya Bongo kila kukicha hivyo anastahili kuishi maisha ya kistaa kuliko msanii mwingine yeyote kwa sasa.

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

NI ZAMU YA ZUCHU

“Mambo hayo tulizoea kuyaona kwa Wema, Uwoya au Hamisa, lakini sasa ni zamu ya Zuchu.“Mtoto anateleza tu na kila siku amekuwa gumzo kwa muziki wake kuandika rekodi mpya Afrika Mashariki.

Irene Uwoya.

NI MIEZI MITANO TU

“Ni miezi mitano tu tangu atambulishwe kwenye muziki, lakini habari zake zinapenya mpaka nje ya Bongo, ambako si rahisi kwa msanii mdogo kama yeye (Zuchu) kufika kwa haraka kiasi hicho.

 

KUKUBALIKA NA KUTEKA SOKO

“Ukiacha kukubalika mwenye au tayari amefikisha wafuasi (subscribers) zaidi ya laki 4.3 kwenye chaneli yake ya Mtandao wa YouTube?“Wewe fuatilia, mitandao yote ya muziki kama Boomplay Music, Audiomack, Apple Music, iTunes, Spotify, Deezer, Tidal, Pandora, Mdundo, Amazon Music na mingineyo, Zuchu amesikilizwa na watu zaidi ya milioni 20. Siyo mchezo…” Anasema mmoja wa wadau hao aliyeomba hifadhi ya jina.

Hamisa Mobetto.

MSANII WA KUTAZAMWA ZAIDI

Hivi karibuni, Zuchu alitajwa na jarida moja nchini Kenya na mtandao wa kuuza muziki duniani, Apple Music kama mmoja wa wasanii wa kutazamwa zaidi barani Afrika.

Gift Stanford ‘Gigy Money’.

REKODI YA LITAWACHOMA NA CHECHE

Wakati hayo yakiendelea, Zuchu ameendelea kuweka rekodi mpya kupitia kolabo zake mbili na bosi wake, Diamond au Mondi za Litawachoma na Cheche, nyimbo ambazo zimesikilizwa (audio) na kutazamwa (video) na mpaka na viongozi wakuu wa nchi kama vile Rais Dk John Pombe Magufuli, Zuchu amefanikiwa kuliteka soko la mtandao.

 

“Ukichungulia kwenye mitandao ya kusikiliza, kutazama, kununua, kuuza na kupakua muziki ya ndani na nje ya Tanzania, utaona ni jinsi gani Zuchu amekuwa na nguvu kubwa kwa kila ngoma anayoachia tofauti na wasanii wengi wapya.

Elizabeth Michael ‘Lulu’.

“Wewe fikiria, ni msanii gani wa kike zaidi ya watu milioni 10 kwa wiki moja.Nyimbo hizo zimeweka rekodi hizo za kipekee, ambazo zinaweza kuchukua muda mrefu kuvunjwa na msanii mwingine aliyepo au atakayekuja, lakini kwa waliopo kwa sasa, wamefunikwa kwa kila namna.

 

ZUCHU ANABEBWA?

Zuchu aliyesainiwa ndani ya WCB Aprili 8, mwaka huu, ni msanii ambaye amefanikiwa kuwa na menejimenti makini inayomsimamia, kiasi cha kutajwa kuwa ndiyo inayombeba.Imeelezwa kwamba, menejimenti hiyo ndiyo inayomvusha kwenye msitu wa sanaa chini ya Mondi, ambaye tayari amevuka mstari wa mafanikio na anaishi maisha ya kistaa kuliko msanii mwingine yeyote Bongo.

 

ZUCHU ANASEMAJE?

Kuhusu mafanikio yake, Zuchu anasema kuwa, kuna nyakati alikata tamaa, lakini alivumilia kuwepo WCB baada ya kuona baadhi ya wasanii alioingia nao wanafanya vizuri, hivyo anamshukuru Mungu kwa kila jambo, kisha Mondi ambaye amempa fursa ya kuwa staa mkubwa Afrika Mashariki.

STORI: SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply