The House of Favourite Newspapers

Wafugaji Wamshambulia Mwenyekiti

0

 

WATU zaidi ya 20 ambao ni jamii ya wafugaji wanadaiwa kumshambulia Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha, kwa kumpiga kichwani, mkononi kwa kutumia fimbo na vitu vyenye ncha kali na kuwa sababishia majeraha wakati akiwa shambani.

 

Tukio hilo limetokea wakati Chacha, mgambo na baadhi ya maofisa wa CHAURU wakielekea katika eneo la shamba lao lililopo Ruvu ambalo wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao mara kwa mara na kuharibu mazao yaliyolimwa.

 

Inaelezwa kuwa baada ya kufika shambani mgambo walipoona kundi hilo la wafugaji waliamua kukimbia kwa hofu, ndipo wafugaji hao wakapata fursa ya kumvamia Chacha na Afisa kilimo wa CHAURU Mwita Daniel.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Visezi Halmashauri ya Chalinze Mohamed Musa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema wafugaji kulisha mifugo kwenye shamba hilo imekuwa kawaida kwao hasa kipindi cha kiangazi.

Leave A Reply