Wafungwa 79 Gereza Butimba Waliosamehewa na Rais Waachiliwa
Leo Desemba 10, wafungwa 79 wameachiwa kati ya wafungwa 190 waliopewa msamaha na Rais Dkt. John Magufuli kwa mkoa wa Mwanza huku sababu kuu ya kuachiliwa idadi hiyo ni kwasababu wengine hawajakidhi vigezo vya kunufaika na msamaha huo.
Wafungwa wa kike Gereza Kuu Butimba – Sehemu ya Wanawake wakitoka gerezani baada ya Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru.
Rais Magufuli jana alitoa msamaha kwa wafungwa 5,533.
Wafungwa 79 wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na msamaha wa Rais waachiliwa leo Desemba 12, 2019 Jijini Mwanza.