Waje: sina haraka ya kuolewa

Waje-BioMwimbaji maarufu wa Nigeria, Waje.

MWIMBAJI maarufu wa kike nchini Nigeria, Waje, amesema hana haraka ya kuolewa na jambo hilo litatimia wakati wake ukifika.

Amesema hivi sasa amaelekeza nadhari yake katika muziki na kumhudumia binti yake ambaye alimzaa akingali na umri mdogo na hataki kubabaishwa na maneno ‘Nakupenda’ ambayo husemwa na wanaume kwa wanawake kila mara.

Kwa maoni yake, maneno hayo hivi sasa yanatumika kama silaha ya kuwalaghai wanawake badala ya kuonyesha upendo wa kweli.

Loading...

Toa comment