The House of Favourite Newspapers

Wakala wa Gvardiol Akanusha Kuwepo kwa Makubaliano ya Awali na Klabu Yoyote

0
Mlinzi wa kati wa RB Leipzig na timu ya Taifa ya Croatia, Josko Gvardiol

WAKALA wa Beki wa kati wa Timu ya Taifa ya Croatia pamoja na klabu ya RB Leipzig Josko Gvardiol anayeitwa MarjanSisic amekanusha uvumi unaoenea kuwa mteja wake tayari ameshasaini mkataba wa awali na klabu moja kwa ajili ya kujiunga nayo majira ya usajili wa kiangazi mwaka 2023.

 

Sisic amenukuliwa akisema kuwa:

“Kuhusu uwezekano wa uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka 2023, hatuna haraka, na naweza kuweka sawa hili suala kuwa hatuna makubaliano ya awali na klabu yoyote ile.

Ukweli ni kwamba vilabu vingi vikubwa vimenipa taarifa kuhusu Josko, lakini bado ana mkataba mrefu na Leipzig. Josko anajisikia furaha sana Leipzig. Maendeleo yake yanashangaza sana na RB wanacheza vizuri chini ya Marco Rose.

Josko Gvardiol

Kumekuwa na taarifa kuwa klabu ya Chelsea huenda ikawa mbioni kukamilisha usajili wa Gvardiol, beki mwenye umri wa miaka 20 na ambaye ni tegemeo katika safu ya Ulinzi ya timu ya klabu ya RB Leipzig na timu taifa ya Croatia ambayo tayari imeshatinga katika hatua ya makundi ya mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar.

 

Vilabu vingine vinavyohusishwa na nia ya kumnasa nyota huyo ni pamoja na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania na klabu ya Paris Saint Germain ya nchini Ufaransa.

 

Thamani ya beki huyo kwa sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya kitita cha paundi milioni 80.

 

 

 

Leave A Reply