The House of Favourite Newspapers

Wakali wa Movies za Global TV Watajwa Tuzo za SZIFF 2019

Magreth.

UNAWEZA kuingia katika Mtandao wa YouTube ukatumia bando na muda wako kuangalia video nyingi na usikate ile kiu yako kutokana na kitu kimoja tu, yaani filamu nzuri za Kibongo!

 

Bado hujachelewa na usilalamike kiviiile kwani TV namba moja Online ya Global inayobamba kwa habari za burudani, siasa na kijamii ndani na nje ya Bongo ina kila sababu ya kukata kiu yako kupitia filamu kabambe za Bongo, Chanzo Ni Wewe pamoja na Coretha.

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART ONE)

 

Kama ulikuwa hujui, filamu hizo ambazo huoneshwa na TV hiyo kila Jumamosi saa 5:00 Asubuhi ni bora kuanzia picha hadi wahusika na zimefanikiwa kupita bila zengwe katika tuzo kubwa za filamu nchini za Sinema Zetu maarufu kama SZIFF (Sinema Zetu International Film Festival).

Washiriki wakuu wa filamu hizo, Emmanuel Maasa, Magreth Francis na Rhoida Richard wamenena juu ya kuingia katika tuzo hizo.

Maseke

“Tunafarijika sana kuona kuwa tupo bora hadi kuingia katika tuzo hizi ambazo ni kubwa sana nchini, kikubwa mashabiki wasisahau kuendelea kutazama filamu zetu zilizojaa ubunifu wa hali ya juu. Naomba kura zenu ili niweze kuibuka Msanii Bora wa Kiume.

 

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART TWO)

Nenda sehemu ya meseji katika simu yako, andika BM kisha acha nafasi andika 1000, acha nafasi kisha andika *8 na utume kwenda namba 0683 520006 utakuwa umenipigia kura,” alisema Emmanuel Maasa aliyecheza Filamu ya Coretha.

Naye Rhoida aliyecheza Filamu ya Ardhi ya Damu aliwaomba mashabiki na wapenda filamu za Kibongo kwa ujumla kumpigia kura katika tuzo hizo.

Rhoida

“Jinsi ya kunipigia kura katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike, nenda sehemu ya kuandikia meseji andika BF acha nafasi kisha andika 760, acha nafasi andika *9 kisha tuma kwenda namba 0683 520006 utakuwa umefanya poa sana,” alisema Rhoida.

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART ONE)

Kama ilivyo katika kutazama na ukaipenda, kura yako pia muhimu ili filamu na washiriki wake washinde katika tuzo hizi.

Surej

Kupigia kura Filamu Bora ya Mwaka kupitia Filamu ya Ardhi ya Damu andika 760 kisha acha nafasi, andika *9 na tuma kwenda 0683 520006.

Filamu ya Chanzo Ni Wewe andika 360 kisha cha nafasi, andika *7 na utume kwenda 0683 520006.

Filamu ya Coretha andika 1000 kisha acha nafasi, andika *8 na utume kwenda 0683 520006.

 

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART TWO)


Kumbuka tuzo hizi ni za pili kufanyika na ni tuzo kubwa na za kwanza za filamu nchini. Bado hujachelewa unaweza pia kuwa mwanafamilia wa Global TV Online kwa kuingia katika Mtandao wa Youtube na kutafuta neno Global TV kisha una-subscribe ili usipitwe na kutafuta filamu za Kibongo. Enjoy!

MWANDISHI WETU

Comments are closed.