The House of Favourite Newspapers

Wakimataifa, Kazi na Iendelee Caf

0

WIKIENDI iliyopita ilikuwa tamu na chungu kwa wadau mbalimbali wa soka hapa nchini kufuatia michezo ya kwanza ya hatua ya awali ya michuano ya kimataifa.

 

Yanga walikuwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Biashara United na Azam wao wakianza kuzicheza karata zao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Hongera kwa Azam na Biashara ambao walianza vizuri kwa ushindi, Azam wao wakiwa nyumbani walishinda mabao 3-1 dhidi ya Horseed ya Somalia, huku Biashara wao wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Dikhil katika ardhi ya Djibout.

 

Yanga wao wakiwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, walidondokea pua baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

 

Michezo hiyo ya mkondo wa kwanza ni kama dakika 45 katika mchezo wa dakika 90, hivyo hampaswi kubweteka bali ni wakati wenu kuhakikisha dakika 45 za kipindi cha pili zinakuwa zenye maamuzi sahihi kwa taifa letu.

 

Yanga bado mna nafasi kubwa ya kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano kule Nigeria kama mtachanga karata zenu vizuri, lakini Azam na Biashara ni muhimu kujitahidi kumaliza kazi ambayo mliianza.

Leave A Reply