The House of Favourite Newspapers

Waliochanjwa Corona Hakuna Aliyefariki

0

Utafiti uliofanywa na wanasayansi nchini Uganda umebaini kuwa chanjo ya UVIKO-19, imepunguza vifo vya corona nchini humo.

 

Matokeo ya utafiti huo yameonesha kwamba hakuna hata mgonjwa mmoja wa corona ambaye alipata chanjo kamili na alipoteza maisha.

 

Hata hivyo kumekuwa na vifo vichache kwa wagonjwa ambao walikuwa hawajakamilisha chanjo kamili ya UVIKO-19.

 

Utafiti huo umefanyika kati ya Mei na Julai mwaka huu ukitumia takwimu za wagonjwa 1,462 waliolazwa katika kituo kikuu cha matibabu ya corona Jijini Kampala.

 

Baadhi ya watu nchini Uganda wamepata chanjo kamili na wengine wamepata chanjo ya dozi ya kwanza ya AstraZeneca, ambayo ndiyo chanjo pekee iliyopo nchini Uganda kwa wakati huo ambayo hutolewa kwa dozi mbili.

Leave A Reply