The House of Favourite Newspapers

Waliochanjwa Kenya Kuchanjwa Tena

0

WIZARA ya Afya ya Kenya imezishauri hospitali kuacha kutoa dozi ya kwanza ya chanjo ya AstraZeneca kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19) kwa wananchi.

 

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe anasema shehena ya chanjo inayowasili nchini humo hivi leo kutoka Covax imemekusudiwa wale wanaostahili dozi ya pili ya chanjo hiyo.

 

Zaidi ya Wakenya 950,000 ambao waliopokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 katikati ya Machi watapokea dozi ya pili kuanzia leo.

Waziri Mutahi amesema chini ya hali ya sasa itakuwa bora kuhakikisha kuwa watu hao wamepewa chanjo kamili ili kujikinga na maambukizi ya Covid-19.

 

Dozi moja ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca inatoa karibu 70% ya kinga kwa angalau wiki 12 na asilimia 81 baada ya dozi kamili.

 

Aidha, Waziri Mutahi alisema wale ambao bado hawajachanjwa watapewa chanjo zingine kama vile Johnson na Johnson. Walakini, bado haijulikani ni lini itawasili.

 

Leave A Reply