The House of Favourite Newspapers

Watia Nia Ubunge CCM Jimbo la Hai Waja Na Jambo Lao

0
Shabani Mwanga akizungumza na wanahabari leo.

Aliyekuwa mtiania wa kugombea Ubunge Jimbo la Hai kupitia CCM, Shabani Mwanga, leo ametangaza rasmi kuanza kuungana na mgombea aliyepitishwa na chama hicho katika jimbo hilo, Saashisha Mafuwe.

Mgombea Ubunge Jimbo la Hai kupitia CCM, Saashisha Mafuwe.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo, Mwanga amesema hilo ndilo jambo lao yeye na wenzake 41, waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho wamekubaliana kiroho safi kumsaidia Saashisha ili kumuondoa maradakani mbunge wa Chadema, Freeman Mbowe aliyekaa kwenye jimbo hilo miaka 15 sasa.

Mwanga amewataka wananachi wa Jimbo hilo kumchagua Saashisha kwa ajili ya maendeleo ya haraka katika jimbo hilo na kuwataka wananchi hao kumchagua Dkt. John Pombe Magufuli katika nafasi ya uraisi ili aendeleze mazuri yasiyo na mfano aliyofanya ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano aliyokaa madarakani.

Dkt. John Pombe Magufuli alipozindua rasmi kampeni za uchaguzi Mkuu Jijini Dodoma hivi karibuni.

Ameendelea kusema kuwa jimbo hilo limekuwa nyuma kwa muda mrefu kutokana na kuongozwa na Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema na amekuwa akitumia muda mwingi kukipigania chama chake na kulisahau jimbo. Alisema Mwanga.

Sehemu ya mapaparazi walipokuwa kazini kumsikiliza Shabani Mwanga leo.

HABARI/PICHA: MWANDISHI WETU

Leave A Reply