Waliomuita Darleen Mgumu Wameumbuka

FIRST lady wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amesema, waliokuwa wakimuita mgumu, sasa wameumbuka baada ya kufunga ndoa hivi karibuni.

 

Akipiga stori na Showbiz, Darleen amesema anamshukuru Mungu kwa kumpa mume maana watu wengi walikuwa wakimfikiria tofauti kwamba siyo mwanamke wa kuolewa na kumtolea maneno mabaya kuwa ni mgumu, hivyo wameumbuka.

 

“Jamani wale waliokuwa wakiniita mgumu wako wapi? Ni hivi, kila jambo na wakati wake, namshukuru Mungu amenijaalia mume na mimi ni mke wa mtu sasa. Wale wenye fikra potofu, wajue wa-kati wa-ngu sasa umefika, wao wabaki hivyo-hivyo,” amesema Queen Darleen ambaye ni dada wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond.

IMELDA MTEMA

 

Toa comment