The House of Favourite Newspapers

Waliopigwa ‘Stop’ Yanga Kukiona Chamoto

SPOTI Xtra limejiridhisha kwamba wachezaji wanne waliopigwa stop kwa makosa ya kinidhamu watakatwa mshahara kwa amri ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera.

 

Wachezaji ambao wamesimamishwa kwa utovu wa nidhamu ni pamoja na kipa Ramadhan Kabwili, Pius Buswita, Said Makapu pamoja na Haji Mwinyi.

 

Habari za ndani kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema kuwa nyota wa timu hiyo ambao wamesimamishwa kama Kabwili ambaye alikosekana kambini siku nne atakatwa mshahara wake na hao wengine wata-fanya maz-oezi mara mbili ambayo watakuwa wanafanya wenzao.

 

“Kabwili yeye ni lazima akatwe mshahara kutokana na utovu wa nidhamu ambao aliony-esha na hawa wengine wanaadhabu zao ambazo ni pamoja na kufanya mazoezi mara mbili ya wenzao,” kilisema chanzo.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera alisema:“Wachezaji wetu wanatakiwa kubadilika kuwa na nidhamu kama wanahitaji kufanikiwa na kufika mbali.”

Comments are closed.