The House of Favourite Newspapers

Wamekopi na kupesti kutoka kwa hawa!

0

AUNT NA IYOBOMakala: Boniphace Ngumije

IMEZOELEKA kuwa kwa kawaida, mwanaume anapaswa kumzidi umri mpenzi wake wa kike. Hili limekaa vizuri na linakubalika kila sehemu, lakini inapotokea mwanamke akawa mkubwa kuliko mwanaume wake, huonekana siyo jambo la kawaida na manenomaneno huwa mengi.

Wapo mastaa kadhaa ambao uhusiano wao wa kimapenzi umeleta gumzo kutokana na kutofautiana umri, wengine wakikejeliwa kwa ‘kuwabemenda’ ma-‘serengeti boys’ wao.wema na idris 2

Baadhi ya ‘kapo’ za wasanii hao ni Densa Moses Iyobo (23) ambaye mama wa mtoto wake, Aunt Ezekiel anadai kuwa na umri wa miaka 26.

Yupo pia Wema Sepetu (27) anayetajwa kutoka na Idris Sultan (23) ambaye ni mdogo kwake kiumri, Nuh Mziwanda aliyekuwa akitoka na Shilole kabla ya kuachana au kama walivyo sasa, dogo wa Bongo Fleva Harmonize anayetoka na mkongwe wa filamu, Jacqueline Wolper.

Harmonizer-na-WolperKule majuu, utamaduni huu ulianza zamani na unaendelezwa kama mastaa wafuatao wanavyothibitisha.

Meek-Mill-Nicki-MinajMeek Mill na Nick Minaj

Robert Williams ‘Meek Mill’ ni rapa kutoka Marekani ambaye yuko chini ya lebo ya Maybach Music na kwa sasa anatoka na mwanadada mwenye jina kubwa kwenye tasnia ya burudani duniani, Onika Maraj ‘Nicki Minaj’ ambaye anamzidi takriban miaka 4, akiwa na miaka 33 huku Meek Mill ana 29.

wiz-khalifa-amber-rose-divorce-gty-ftrWiz Khalifa na Amber Rose

Wawili hawa enzi za uhusiano wao walitengeneza sana vichwa vya habari za burudani kutokana na mvuto waliokuwa nao kwa mashabiki. Wiz Khalifa ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 28, akiwa amezaa na mrembo huyo mtoto wa kiume aitwaye Sebastian Thomaz, amezidiwa miaka minne. Baada ya kumwa-gana, hivi sasa Amber anatoka na mcheza kikapu Terrence Ross.

tyga-blac-chyna-last-kingsTyga na Blac Chyna

Mkali wa michano Tyga 26 anaingia katika orodha hii akiwa na mwanadada asiyekaukiwa vituko Blac Chyna, 28 ambaye ni mama wa mtoto wake aitwaye King Cairo Stevenson. Hata hivyo, wawili hawa ambao wanazidiana miaka miwili wamekwisha achana, Tyga kwa sasa anatoka na mwanamitindo Demi Rose huku Blac Chyna akiwa na Rob Kardashian, ndugu wa mwanamitindo maarufu Kim Kardashian.

attends the 2008 Whitney Museum of American Art's gala and studio party at the Whitney Museum of American Art on October 20, 2008 in New York City.
attends the 2008 Whitney Museum of American Art’s gala and studio party at the Whitney Museum of American Art on October 20, 2008 in New York City.

Nicholas Cannon na Marieh Carey

Cannon ambaye ni rapa, muigizaji na mchekeshaji alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kuanzia mwaka 2008 na mwanadada mwenye heshima kubwa katika Tasnia ya Muziki wa RnB, Mariah Carey ambaye baadaye walioana na kubahatika kupata watoto wawili Monroe na Morroccan kabla ya kuachana mwaka 2015.

Japo wawili hao walikuwa wanazidiana zaidi ya miaka 8, Mariah Carey akiwa na miaka 46 huku Cannon akiwa na 35 kwa sasa, lakini uhusiano wao ulikuwa na mvuto sana kwenye

Leave A Reply