Wamiliki wa Malori Wawaweka Mtu Kati, Tanrod, TRA, LATRA, EWURA
CHAMA cha wamiliki wa malori wadogo na wakati nchini TAMSTOA kimeziweka mtu taasisi za serikali wanazofanya nazo kazi na kuwapa changamoto wakiwemo Mamlaka ya Mapato nchini TRA, LATRA, Tanrod, EWURA na Jeshi la Polisi.
TAMSTOA iliwaweka kikaangoni wadau wake hao kwenye mkutano wao mkuu wa pili uliofanyika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel jijini Dar Alhamisi iliyopita.
Katika mkutano huo ambao wamiliki hao wa malori waliwaalika wadau mbalimbali waliwaelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji wao wa kazi.
Akizungumzia changamoto zinazowakabili kwenye uendeshaji wa shughuli zao Mwenyekiti cha chama hicho Chuki Shabani alizitaja baadhi yake kuwa ni upandaji bei za mafuta kiholela, magari yao kukamatwa bila sababu za msingi, kutozwa kodi nyingi tofauti na wenzao wa nchi jirani jambo linalosababisha baadhi ya Watanzania kuyasajili malori yao nchi hizo ili kukimbia kodi kubwa zinazotozwa hapa nchini.
Akizungumza na wanahabari msemaji wa Mjumbe Wa Kamati Kuu ya TAMSTOA na Msemaji wa chama hicho, Mark Gama ameiomba serikali kuwapunguzia changamoto hizo ili waendelee kufanya shughuli zao kiufanisi na kuweza kulipa mapato ya taifa.
Gama pia ametumia nafasi hiyo kiumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuingilia wana popatwa na matatizo kaka hivi karibuni alivyowasaidia katika sakata la madereva wao waliobeba magogo walivyokamatwa nchini Zambia.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL