The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi 13 wa Marekani Wauawa Afghanistan

0

SHAMBULIO kubwa limetokea jana Alhamisi, Agosti 25, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kabul nchini Afghanistan na kusababisha vifo vya watu 60 na 140 kujeruhiwa katika milipuko miwili.

 

Wanajeshi 13 wa Marekani ni miongoni mwa waliokufa, Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, Pentagon imethibitisha, katika siku inayoonekana kuwa mbaya zaidi kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan tangu mwaka 2011.

 

Akijibu shambulio hilo, Rais wa Marekni Joe Biden amewaambia waliohusika: “Tutawasaka na kulipiza”
Anaapa pia kumaliza oparesheni ya kuwaokoa watu, lakini amesema kwamba “kumtoa kila mtu nje sio jambo ambalo anaweza kutoa hakikisho”

Rais anasema hadi sasa hakuna uthibitisho wa ushirikiano kati ya Taliban na Dola la Kiisilamu, Isis-K ambalo alidai kuwa ndilo lililosababisha shambulio hilo.

 

Viongozi wa nchi za Magharibi wamelaani shambulio la Kabul, kwani mataifa kadhaa yanamaliza shughuli zao za uokoaji

 

Makamanda wa Marekani wako macho juu ya hofu ya mashambulio zaidi Kutoka kwa ISIS, pamoja na roketi zinazowezekana au mabomu yanayosafirishwa kwa gari yakilenga uwanja wa ndege wa Kabul, mkuu wa Jeshi la Marekani Frank McKenzie alisema.

“Tunafanya kila tuwezalo kuwa tayari,” Jenerali McKenzie alisema, wakati vikosi vya Marekani vikilenga kumaliza kujiondoa kwao Afghanistan.Marekani inharakisha kukamilisha uokoaji kufikia tarehe ya mwisho – 31 Agosti iliyokubaliwa na Taliban.

 

Rais wa Markani Joe Biden hajazidisha muda wa oparesheni hiyo .Alhamisi jioni alisema kuwa juhudi za uokoaji zitaendelea licha ya mashambulio hayo.

Leave A Reply