The House of Favourite Newspapers

Wanaodaiwa Majambazi Sugu Wanaswa

0

JESHI la Polisi Mkoani Tanga limewakamata watu wanne wanaodaiwa kuwa ni Majambazi sugu waliokuwa wakitafutwa kwa muda mrefu katika wilaya ya Korogwe akiwemo kiongozi wa genge la uhalifu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tanga na nje ya mkoa na mlinzi wa kampuni ya Gomba Estate.

 

 

Watu hao wamekamatwa mwishoni mwa wiki katika oparesheni ya Kikosi maalumu cha jeshi hilo usiku wa kuamkia Januari 25 katika eneo la kibaoni Mombo wilayani Korogwe ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amewataja watu hao kuwa ni Hamis Mbelwa (46), Haji Semkondo,(42), Barnaba Simon (62)na Ally Babiwi wote ni wakazi wa Korogwe.

 

“Hamis Mbelwa alikuwa mfungwa katika gereza kuu la mkoa wa Tanga Maweni, alihukumiwa miaka 30 jela mwaka 2015 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha huko Korogwe na alitoroka gerezani na kuungana na genge lake la uhalifu Juni 2019.

 

 

“Walifanya uporaji wa kutumia silaha hospitali ya Rosmin wilayani Korogwe na kufanikiwa kupora Shilingi milion 8.0. Barnaba Simon Maarufu kwa jina la Nyau Spos, alikuwa mlinzi kampuni ya Gomba Estate wilayani Korogwe lakini ni mshirika wa genge la uhalifu lililokuwa likiongozwa na Hamis Mbelwa.

 

 

Watuhumiwa wamekuwa wakitumia silaha aina ya Shotgun yenye usajili wa 328932 silaha ambayo hutumika kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu, “Huyu ni mlinzi lakini pia ni mshirika wa genge la uhalifu la Hamis Mbelwa na amekuwa akiwakodishia silaha majambazi wenzake kwa ajili ya utekelezwaji wa uhalifu,” alisema Chatanda.

 

 

Haji Semkondo na Ally Juma ambao waliokuwa ni washirika wa genge hilo wamekuwa wakifanya uhalifu kwa kutumia silaha, utekaji barabarani katika Barabara kuu ya Tanga -Arusha na unyang’anyi wa kpikipiki. Chatanda alisema msako wa kuwatafuta wahalifu wengine waliosalia.

Leave A Reply