The House of Favourite Newspapers

Wanasayansi Watahadharisha Mlipuko wa Volkano DR Congo

0

WANASAYANSI wametahadharisha kuhusu hatari ya Mlima Nyiragongo uliopo Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo kulipuka.

 

Mlima huo ulilipuka kwa Volkano Januari 2002, na kusababisha vifo vya watu 250 na uharibifu wa 20% ya Mji wa Goma.

 

Dario Tedesco, Mtaalamu wa Volkano na Milima amesema ipo hatari ya mlima huo kulipuka tena. Na itakuwa ni ya hatari zaidi duniani.

 

Tathmini inaonesha kuwa hatari kubwa zaidi ya mlima huo itatokea ndani ya kipindi cha miaka 4, lakini tetemeko la ardhi linaweza kusababisha mlipuko mapema zaidi.

Leave A Reply