The House of Favourite Newspapers

Warundi 7 Jela kwa Kuingia TZ Kinyemela

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia saba wa Burundi kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi laki tano kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega.

 

Katika hatua nyingine mahakama hiyo imewahukumu vijana wawili faini ya shilingi milioni tano au kifungo cha mwaka mmoja  kwa kosa la kuchapisha maudhui mtandaoni bila leseni ya TCRA.

 

Watu hao, Emmanuel Sisala na Juhudi Motela, wanadaiwa kati ya Januari 2018 na Februari 2020 ndani ya jiji la Dar es Salaam kupitia televisheni yao ya mtandao ijulikanayo kama Jumo Online TV walitoa maudhui mbalimbali bila kuwa na leseni.

Kabla ya hukumu hiyo, upande wa mashtaka kupitia Wakili wa Serikali, Adolf Lema,  aliomba vifaa ambavyo walikutwa navyo vitaifishwe vikiwemo kompyuta na simu.

 

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mbando amesema  washtakiwa wamekiri makosa yao na amewatia hatiani na kutafaisha vielelezo 11 ikiwemo komputa aina ya Apple, simu tatu, vinasa sauti na kamera.

 

Leave A Reply