The House of Favourite Newspapers

Wasanii Wa Kike Wenye Wafuasi Wengi Youtube

0

YOUTUBE ni moja kati ya mitandao ambayo kwa kiasi kikubwa inatoa kipimo halisi cha kazi za wasanii. Kupitia mtandao huo unaweza kujua nani ametazamwa zaidi, wimbo gani umefanya vizuri zaidi kutokana na jinsi watu wanavyotazama kazi husika.

Kuna baadhi ya wasanii wanaachia ngoma haziendi kwenye trending kwa maana ya kushika namba moja, mbili au tatu lakini wapo ambao kila wakitoa lazima nyimbo zao zifike namba moja. Hiyo inatokana na jinsi ambavyo wimbo au msanii husika anavyokubalika.

Hapa leo nakuletea orodha ya wasanii ambao wanaongoza kwa kuwa na watu wengi wanaowafuata (subscribers) kwenye mtandao wa YouTube.

 

Unapokuwa na subscribers wengi maana yake pia una wigo mpana wa kuwa na mashabiki wengi, inaonesha ni jinsi gani muziki wako unakubalika:

 

ZUCHU

Mrembo huyu kutoka pale Wasafi Classic Baby (WCB) ndiye anayekama usukani kwa sasa Bongo kwa kuwa na subscribers wengi zaidi kwenye akaunti yake ya YouTube ambapo anao Milioni 1. 03.

Zuchu ambaye hana muda mrefu kwenye gemu, ameibuka na kuwakuta wasanii wengi wakongwe lakini ndani ya muda mfupi amekaa kileleni.

NANDY

Huyu ndiye unaweza kusema ndiye mshindani halisi wa Zuchu kwa sasa kwania anakamata nafasi ya pili akiwa na wafausi wasiopungua 728,000. Nandy yeye alikuwepo muda mrefu kabla ya Zuchu kuibuka kwenye gemu lakini kutokana kabinti hako kutoka Wasafi kamekuja na nyota yake na kufanikiwa kumuacha vibaya.

 

VANESSA

Huyu alianza gemu kitambo kidogo lakini akaipa kisogo na kutimkia zake Marekani anakoishi na mpenzi wake Rotimi. Lakini kabla hajaondoka nchini, muziki wake ulikuwa unapendwa na alikuwa anaongoza kwenye chati za wasanii wa kike mara kadhaa.

Licha ya kuondoka nchini na kuacha muziki kwa muda, bado ameendelea kukamata nafasi ya tatu kwenye Top Five hii kwani anao subscribers 276,000. Kama angekuwa bado anaendelea kufanya muziki basi pengine angekuwa juu zaidi ya hapo alipo.

HAMISA MOBETO

Unaweza usiuone sana uwezo wake kwenye muziki lakini ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wanafanya vizuri kwenye YouTube kwani anao subscribers 126,000 hivyo anakamata nafasi ya nne kwenye chati hii.Hamisa ni mchanga sana kwenye gemu lakini mwendo wake unaridhisha, kama ataendelea kukaza buti na akawa serious na muziki, huwenda akafika mbali zaidi.

 

LADY JAYDEE

Unapozungumzia wanamuziki wakongwe ndani ya nchi hii huwezi kuacha kumtaja mkali huyu aliyedumu kwenye gemu kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Lakini pamoja na ukongwe wake, bado kwenye chati hii ameachwa kidogo na wadogo zake kwani yeye anao subscribers 88,000 na anakamata nafasi ya tano. Hivyo anahitajika kufanya jitihada za makusudi kama kweli anataka kuonesha ukongwe wake kwa wadogo zake.

MAKALA NA ERICK EVARIST | GPL

Leave A Reply