The House of Favourite Newspapers

Washindi Watatu wa ‘Shinda Nyumba’ Wachukua Zawadi Zao

0
Festo Masigasi (kushoto) mshindi wa simu ya kisasa, akipokea zawadi yake kutoka kwa Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Andrew Carlos.

 

WASHINDI watatu wa droo ya tano ya shindano la ‘Shinda Nyumba’ leo wameondoka na zawadi zao katika ofisi za Global Publishers zlizoko Mwenge-Bamaga jijii Dar es Salaam.

 

Washindi hao ni Ummy Ally kutoka Dodoma ambaye aliwakilishwa na ndugu yake, Judah Rasul, aliyemchukulia zawadi ya vyombo vya nyumbani (dinner set); mwengine ni Festo Masigasi kutoka Bunju ambaye alishinda simu ya kisasa (smart phone) na David Shagalawa ambaye alishinda televisheni ya ukutani (flat screen).

 

 

Kushoto ni Judah Rasul akimwakilisha Ummy Ally wa Dodoma ambaye ni mshindi wa ‘dinner set’, kulia ni mwandishi wa habari wa Global, Nyemo Chilongani akikabidhi zawadi hiyo.

Wakizungumza na gazeti la Amani kwa nyakati tofauti, washindi hao waliishukuru kampuni yaGlobal Publishers kwa zawadi hizo huku wakitoa wito kwa watu wengine kushiriki katika shindano hilo ambalo ni maarufu nchini.

 

 

Restuta Shangalawa akimwakilisha mshindi wa TV  ya kisasa (flat screen), David Shangalawa mkazi wa Kigoma, kulia ni Mr. Shinda Nyumba akibadhi zawadi hiyo.

 

“Naishukuru Global Publishers kwa zawadi hii, hakika nilidhani mambo haya ni ya kupeana lakini ukweli ni kwamba hakuna mazingira ya kupeana, kila mtu anashinda kutokana na bahati yake,” alisema Restuta Shangalawa aliyepokea zawadi kwa niaba ya David Shangalawa, mshindi kutoka Kigoma.

 

 

Washindi wa droo ya 5 wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa masoko wa Global Publishers.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, aliitoa wito kwa wasomaji kuendela kujaza kuponi zilizoko magazetini na kushiriki katika shindano la Shinda Nyumba ambalo linabadilisha maisha ya watu wengi nchini.

“Watu waendelee kujaza kuponi ili wajisogeze kwenye nafasi kubwa ya ushindi kwani shindano hili limebadilisha maisha ya watu wengi sana. Kwa hiyo watu wachangamkie fursa hii,” alisisitiza ofisa huyo.

 

Na Ally Katalambula | GPL

 

Washindi wa Droo ya 5 ya Shinda Nyumba Wakabidhiwa Zawadi Zao

Leave A Reply