The House of Favourite Newspapers

VILIO, SIMANZI VYATAWALA KUAGWA KWA MTOTO NORAH

0
Jeneza lenye mwili wa marehemu.

 

NI huzuni na simanzi kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki iliyoambatana na vilio wakati wa shughuli yaa kuaga mwili wa mtoto Norah Jimmy (11) aliyefariki dunia juzi kwa kile kinachodaiwa kuwa alibakwa kisha kunyongwa.

Wanafunzi wenzake wakiwa katika majonzi.

 

Wanafunzi waliokuwa wakisoma na Norah wameingiwa na simanzi kubwa na kushindwa kujizuia na kuangua vilio baada ya kuona jeneza lenye mwili wa mwenzao alitetangulia mbele za haki.

 

…Wakiangua vilio.

 

Norah aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Atlas iliyopo Ubungo, ameagwa leo nyumbani kwao maeneo ya Sinza Mori jijini Dar na anatarajiwa kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni.

 

Gari lenye mwili wa marehemu likiwasili nyumbani kwao.

 

Inadaiwa mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho cha kikatili cha kubakwa kisha kunyongwa mpaka kufa na mjomba wake aitwaye John Msigala.

 

Mwili wa marehemu ukipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa.

 

Mpaka sasa bado haijatolewa ripoti ya daktari ya kuthibitisha chanzo cha kifo cha Norah,  huku jeshi la polisi likisisitiza waombolezaji wa msiba huo kuvuta subira mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.

 

Hakika ni simanzi.

 

Watoto wenzake wakiangua vilio.

 

Wazazi wa marehemu wakiomboleza (wa pili na watatu kushoto).

 

Waombolezaji wakiwa wenye huzuni.

NA ISRI MOHAMMED | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply