The House of Favourite Newspapers

Wasomaji wa Gazeti la Championi, Mbezi Mwisho, Goba Wajinyakulia Mtonyo wa Mr. Championi

0
Ofisa Masoko wa Gloabal Publishers, Antony Adam (kushoto) akimrudishia fedha yake aliyonunulia gazeti msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Gloabal Publishers, Songoro Bilal (kushoto) akimrudishia fedha yake aliyonunulia gazeti msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Gloabal Publishers, Songoro Bilal (kulia) akimrudishia fedha yake aliyonunulia gazeti msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Gloabal Publishers, Songoro Bilal (kushoto) akimrudishia fedha yake aliyonunulia gazeti msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Gloabal Publishers, Antony Adam akimrudishia fedha yake aliyonunulia gazeti msomaji wa Gazeti la Championi.
Ofisa Masoko wa Gloabal Publishers, Songoro Bilal (kulia) akimrudishia fedha yake aliyonunulia gazeti msomaji wa Gazeti la Championi.

 

IKIWA ni mwezi mmoja sasa umetimia tangu Gazeti namba moja la Michezo na Burudani Tanzania la Championi kuingia mtaani na kuwarudishia fedha yao wasomaji waliokutwa wakisoma gazeti hilo, mapema leo Mr. Championi aliwarudishi fedha walizonunulia gazeti waliokutwa wakilisoma gazeti hilo.

 

Mr Championi huingia mtaani kila siku za jumamosi na kuwarudishia fedha wasomaji ambao wanakutwa wakisoma gazeti hilo ambalo huuzwa kwa Sh 800 tu.Wasomaji mbalimbali wa maeneo ya Mbezi Mwisho na wa maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam wamerudishiwa fedha baada ya kukutwa wakilisoma.

 

Timu ya Maofisa masoko ya Global Publishers ambao ndiyo wachapishaji wa gazeti hilo walipita mitaa mbalimbali ambapo waliokutwa wakisoma gazeti hilo walisema kuwa ofa hiyo ni nzuri na inaleta faraja kwao kwani wanaporudishiwa fedha waliyonunulia inawawezesha kufanyia mambo mengine.

 

“Tunawashukuru sana nyie Global Publishers , hakika hili gazeti nililonunua kwa Sh 800 la Championi nimesoma nimeridhika lakini kama hiyo haitoshi nimerudishiwa fedha niliyotumia kununua gazeti hili, asanteni sana,” alisema mmoja wa wasomaji waliokutwa na Mr Championi.

 

Msomaji kama wewe hujakutana na Mr Championi leo basi Jumamosi ijayo anaweza kuwa mtaani kwako na kukurudishia fedha yako uliyonunulia gazeti. Usisahau kununua gazeti, soma kila kitu na Mr Championi atakurudishia fedha yako.
watumie

Leave A Reply