The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Wasubiri kwa hamu droo ya 3

0

8.Kuponi za Bahati nasibu ya Shinda Nyumba zikiwekwa katika ndoo maalum ya Shinda Nyumba.
BAADA ya kufanyika kwa kishindo kwa droo ya kwanza na ya pili, wasomaji wengi wameonesha kuingojea kwa hamu droo nyingine ambayo itakuwa ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na kampuni inayochapisha Magazeti ya michezo ya Championi pamoja na Magazeti Pendwa ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Risasi na Ijumaa Wikienda, Global Publishers inayotarajiwa kufanyika Machi 30, mwaka huu.

5.Mmoja wa washiriki wa Droo ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba  mkazi wa eneo la Goba mwisho akiweka kuponi yake.Akizungumza na Risasi Jumamosi, Frank Julius mkazi wa Mabibo, Dar alisema kuwa amekuwa miongoni mwa wasomaji wakubwa wa magazeti ya Global na tangu Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba ilipoanza amekuwa akivutiwa nayo na kutuma kuponi nyingi.
10.Mdau wa Gazeti la Championi,Neema Steven akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.“Nimeshakutana na watu zaidi ya wawili wakiongelea bahati nasibu hii na mimi nikasema ngoja nijaribu bahati yangu. Hadi sasa nimeshatuma kuponi zaidi ya 20 na nasubiri najua kabisa nisiposhinda nyumba mwaka huu lazima nishinde zawadi zilizobakia maana nimeona watu wakishinda seti za vyombo, ving’amuzi, simu za mkononi za kisasa na nyingine nyingi,” alisema Frank.

9.Mshiriki wa Shinda Nyumba,Said Bia (kulia) akivalishwa kofia na Ofisa Masoko wa Global baada ya zoezi la kujaza kuponi yake na kushiriki.Naye Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema kuwa droo hiyo ya tatu inayosubiriwa kwa hamu na wasomaji wa magazeti hayo inatarajiwa kufanyika Machi 30, mwaka huu katika Viwanja vya Manzese-Bakhresa jijini Dar ambapo washindi watapata zawadi nono.
7.Mkanda (kulia) akimsaidia mmoja wa washiriki wa Bahati nasibu ya Shinda Nyumba kumjazia kuponi yake.“Kila mfuatiliaji wa magazeti ya Global Publishers anatambua zawadi zinazotolewa kila droo ikifanyika. Droo ya kwanza tulimpata mshindi wa zawadi kubwa ya TV Flat Screen pamoja na King’amuzi cha Ting, Happyness Haule na waliobakia walipata zawadi kama vile seti ya vyombo vya jikoni, simu za kisasa (smart phone), ving’amuzi vya Ting na nyingine nyingi.

1.Mwanahamisi Kasimu (kulia) mkazi wa maeneo ya Goba Dar akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shionda Nyumba.Anayeshuhudia ni Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda.“Katika droo ya pili pia tulishuhudia kwa mshindi kutoka Kibaha, Pwani ambaye ni Lucy Swai aliyejinyakulia zawadi ya Pikipiki ya Skymark huku zawadi nyingine zikitolewa. Kinachotakiwa ni kununua magazeti yanayochapishwa na Global Publishers kisha jaza kuponi na kuituma kwa mawakala ama ofisini kwetu moja kwa moja,” alisema Mkanda.
SHINDA NYUMBA (22)Katika droo kubwa, mshindi atazawadiwa nyumba ya kisasa iliyopo Salasala-Kinondoni jijini Dar es Salaam, ikiwa na samani za ndani. Katika shindano hili watu walio chini ya umri wa miaka 18, ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers hawaruhusiwi kushiriki.

Leave A Reply